Ephesians 5:8-13

8 aKwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru 9 b(kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli), 10 cnanyi tafuteni yale yanayompendeza Bwana. 11 dMsishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni. 12 eKwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini. 13 fLakini kila kitu kilichowekwa nuruni, huonekana,
Copyright information for SwhKC